

Baada ya mapumziko ya siku mbili, kikosi cha Simba leo kimerejea mazoezini kuendelea na maandalizi ya michezo ya ligi inayofuata
Simba imejifua bila ya kocha wake Mkuu Patrick Aussems ambaye amesimamishwa akisubiri maamuzi ya kikao cha Kamati ya Nidhamu na Maadili ambacho kitakaa keshokutwa Alhamisi
Kocha Msaidizi Denis Kitambi pamoja na maafisa wengine wa benchi la ufundi walisimamia mazoezi hayo yaliyofanyika uwanja wa Gymkhana jijini Dar es salaam
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mazoezi hayo, Kitambi amesema wamefanya mazoezi ya kawaida kuweka miili sawa
Amesema bado hawajaandaa program ambayo wataitumia kipindi hiki ambacho ligi itasimama kwa mwezi mzima kupisha michuano ya CECAFA Chalenji
KUPATA HABARI MPYA KILA WAKATI PAKUA APP YA ......SOKA KIGANJANI



0 Comments