Windows

Samatta wa Ulaya, Mashabiki Watanzania

Samatta - Ulaya- Mashabiki -Watanzania-Tunisia-libya-Shomari- Kapombe-uongozi-magoli-michezo blog-mwanasport-mwanaspotisoka-

Ndio upande wa kulia hatuonekani kama tuna mbadala wa Shomari Kapombe, na timu haifahamu nini inakihitaji pale ambapo inakuwa injaribu kuhifadhi uongozi wake wa magoli.

Tulikuwa nchini Libya katika ardhi ya Tunisia tukicheza na Libya, tukafungwa mabao mawili kwa moja.


Hatukuonekena kama tulikuwa na akili ya kushinda, haikuonekana kama Ndayiragije alikuwa na mpango kabambe wa kushinda mchezo huo baada ya kuwa anaongoza goli moja kwa sifuri.


Ndio upande wa kulia hatuonekani kama tuna mbadala wa Shomari Kapombe, na timu haifahamu nini inakihitaji pale ambapo inakuwa injaribu kuhifadhi uongozi wake wa magoli.


Ni ngumu kufanya makubwa kama hili linaendelea lakini ni lazima tujue bado tunaendelea kuwa Tanzania ambayo wananchi wake wana imani kubwa ya kufika mbali kipindi hiki ambacho upepo upo upande wetu.


Lakini wakati mengi yakiwa ni sababu kubwa, kuanzia maamuzi ya kocha mpaka kiwango chetu kwa ujumla ikiwemo kutumia nafasi ambazo tunatengeneza bado kuna jina moja ambalo Watanzania wengi walilitamka zaidi.


Jina ambalo linaaminika kuwa ni jina linalotakiwa kufanya makubwa. Watanzania wanaamini furaha yao ipo kwenye miguu ya Mbwana Samatta, wanaamini Taifa lipo kwenye uwezo wake na kujitolea kwake ni muhimu zaidi kwao.Ni watanzania hawa ambao wanakaa kwa pamoja mbele ya televisheni ili waweze kumshangilia mchezaji wao huyu akiwa na timu ya Genk.


Wanaamini anawahitaji ili afike mbali zaidi, wanaamini ni lazima wamwombee ili afikie ndoto zake ambazo pia ni ndoto za Watanzania waliokuwa wengi.


Watanzania wanampenda na wamekuwa naye tangu alipokuwa TP Mazembe na wanaendelea kuwa naye katika ndoto za kufika kwenye ligi kubwa zaidi pengine ligi kuu ya England.


Baada ya kuonekana hakucheza vyema, Watanzania walikuwa na haki ya kuzungumza, kulalamika na kumweleza wazi kuwa aliwakera.


Watanzania walikuwa na kila sababu ya kusema Samatta umekikosea heshima kitambaa cha unahodha kwa sababusio tu kwamba unawaongoza akina Juma Kaseja na Simon Msuva bali pia kwenye hili unawaongoza watanzania zaidi ya milioni hamsini wanaotaka kuona Tanzania ipo kwenye kilele cha mafanikio ya soka. Sio jukumu rahisi lakini kama umeamua kulibeba basi lazima ubebane na kasheshe zinazoambatana nalo.


Watanzania hawakuwa wakilalamika kwa sababu hawampendi Samatta, au kumwonea mchezaji wao. Malalamiko yao yalikuwa yanatokana na tamaa yenye nia njema na wengi pia wakiamini kuwa hata huku anatizamwa na akifanya vyema inamuongezea nafasi ya kufanya mambo makubwa zaidi na jina lake kuimarika vyema zaidi.


Ni jambo jema pia kuona Samatta kaelewa, ni vyema kaona kuwa anapendwa, ni jambo salama zaidi kuona ameweza kutambua umuhimu wa kelele za Watanzania. Kupitia mitandao ya Kijamii, Mbwana Samatta kaeleza kupokea kwa moyo mmoja na kwamba atabadilika na kuwafurahisha. Hii ndio Tanzania tunayohitaji, nchi ambayo wachezaji lazima watambue nembo na bendera iliyopo kwenye jezi wanayoivaa ina thamani kubwa zaidi.


Hii itasaidia kuwafanya wachezaji wawe wawajibikaji. Itasababisha wachezaji waliolilia malipo ya fedha zao kule Misri wakati wa AFCON, wafahamu kuwa pia Watanzania wana machozi yao kila timu inapofanya vibaya na ni lazima wafanye vyema ndani ya uwanja kwa sababu wanawakilisha ndugu zao huko. Washabiki wa Tanzania hawaamini tena kama wao ni kichwa cha mwendawazimu, hawaamini kama Uganda anawatisha tena, hawadhani kama Rwanda inawazidi.


Hii ndio sababu timu ya Taifa ya wanawake inajaza washabiki kule kwenye uwanja wa Chamazi na washabiki wamechanganyikiwa kuona timu inavyofanya vyema. Hii ndio Tanzania ya sasa ambayo washabiki wana hamasa na wanajua haki ya kama washabiki na wapo tayari kuwawajibisha wachezaji ambao hawafanyi vibaya.


Miaka mingi iliyopita walikuwa wanawawajibisha akina Haruna Moshi, Athumani Idd Chuji kutokana na tabia zao nje ya uwanja. Watanzania walikuwa wanamsema Mrisho Ngassa kwa kukimbia soka la kulipwa, kwa sababu ndoto zilikuwa kuwapata akina Samatta. Wakishapatikana lazima wafahamu kuna maombi nyuma yao yanayowatakia mema hivyo ni jukumu lao kutenda yale yaliyokuwa mema.


Nimefurahi kuona Samatta kalichukulia vyema hili, hajaona kama ametengwa, amegundua kuwa wanaolaumu wanafanya hivyo kwa nia njema. Hii tabia amejifunza, ameitoa Ulaya alipo na anajua sisi tunabaki kuwa Watanzania na sio raia wa Ubelgiji wanaoipenda Genk. Amefahamu Watanzania watafurahi akifanya vyema kote na kuwa mwenye mafanikio zaidi.


Amejifunza kuwa kuna muda washabiki watakupa hata matusi kwa sababu sio kwamba hawakupendi bali kwa sababu wanafahamu kuwa unaweza kufanya zaidi ya hapo. Hii ndio raha ya Ulaya, kuna majina nayahifadhi hapa nyumbani yangesusa na yangeenda kuwatupia majungu washabiki kwenye mitandao.





Post a Comment

0 Comments