Ndayiragije alisisitiza kuhusu Manula na kuelezea kwamba wakati anaichukua Stars kwa mara ya kwanza walikuwa wakijiandaa kucheza na Kenya katika mechi ya kufuzu Chan, alimuita kipa ambaye alikuwa na kikosi cha Simba kilipoweka kambi yake Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa ligi kuu.
KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Mrundi Ettiene Ndayiragije amesema hata akimuita kipa wa Simba Aishi Manula hataweza kuwa chaguo lake la kwanza kama ilivyo kwa Juma Kaseja.
Ndayiragije amesema Kaseja ataendelea kuwa kipa namba moja kutokana na kiwango chake alichokionyesha kwenye mechi alizocheza za timu ya taifa za kufuzu fainali za Chan na Afcon ambazo zote zitafanyika nchini Cameroon.
Ndayiragije alisisitiza kuhusu Manula na kuelezea kwamba wakati anaichukua Stars kwa mara ya kwanza walikuwa wakijiandaa kucheza na Kenya katika mechi ya kufuzu Chan, alimuita kipa ambaye alikuwa na kikosi cha Simba kilipoweka kambi yake Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa ligi kuu.
"Baada ya kuita Manula na kufanya naye mazoezi kwa siku mbili alinifuata na kuniambia kuwa ni mgonjwa na kubwa ambalo amekosa ni muda wa kupumzika kwani hata akiwa anacheza fainali za mataifa Afrika (Afcon), alikuwa anaumwa,"
"Kwa maana hiyo nikamuachia na kumpa ruhusa ya kwenda kupumzika na badala yake nikaamua kumpa nafasi Juma Kaseja ambaye alicheza vizuri katika mechi zote za Chan na Afcon jambo ambalo kwangu anaendelea kuwa chaguo la kwanza mpaka sasa.
"Kingine, Manula aliniambia anaumwa ndio maana sikumuita hata katika mechi za hivi karibuni kwani nilitaka kujiridhisha kweli amepona na anakuja katika timu kucheza na si kuanza kumuangalia kiwango chake tena," alisema Ndayiragije ambaye aliongezea kuwa Manula ni moja ya makipa wazuri waliokuwa hapa nchini.
"Kiwango ambacho ameonesha Kaseja inakuwa ngumu kumuondoa kwenye kikosi cha kwanza na kama nikimuita Manula atakuwa chaguo la pili," aliongezea Ndayiragije ambaye kabla ya kuwa kocha wa Stars amezinoa timu za Mbao ya Mwanza, KMC na Azam zote za hapa nchini.
0 Comments