Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Etienne Ndayiragije amemtaka beki wa kulia wa Simba Shomari Kapombe kufikiria upya uamuzi wake wa kustaafu kuichezea timu ya Taifa
Ndayiragije amesema bado mchango wa beki huyo mahiri wa pembeni unahitajika hivyo amemuomba arudi kuitumikia Stars
Mwezi uliopita Kapombe alitangaza kustaafu kuchezea timu ya Taifa kutokana na sababu za kiafya
Hata hivyo alisema ataweza kurejea kuitumikia timu hiyo baadae pale changamoto zinazomkabili zitakapokuwa zimemalizika
Msimu uliopita Kapombe alipata majeraha wakati akiitumikia timu ya Taifa. Ni majeraha hayo ambayo yalimuweka nje kwa zaidi ya miezi saba na kutishia hatma yake ya kuendelea kusakata kabumbu
Amekuwa akirejea katika kiwango chake taratibu lakini ameendelea kuchukua tahadhari kuhakikisha hatoneshi majeraha hayo
0 Comments