Windows

Bocco apelekwa Afrika Kusini



Nahodha wa Simba John Bocco amepelekwa Afrika Kusini kufanyiwa uchunguzi zaidi wa jeraha linalomsumbua

Wakati huu ambao ligi itasimama kupisha michuano ya Chalenji, uongozi wa Simba umechukua hatua kuhakikisha mshambuliaji huyo anapona na kuwa tayari kurejea dimbani baada ya mapumziko hayo mwezi January 2020



Hivi karibuni Bocco alianza mazoezi mepesi kwenye kikosi cha Simba baada ya kuwa nje kwa zaidi ya miezi mitatu

Mara ya mwisho Bocco kuitumikia Simba ilikuwa August 17 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam Fc

Ni katika mchezo huo ambao alipata majeraha ya goti yaliyomuweka nje mpaka leo

KUPATA HABARIHIZI KWA HURAHISI PAKUA APP YA >>SOKA KIGANJANI

Post a Comment

0 Comments