

Mabadiliko yameanza kuonekana kwenye kikosi cha Yanga tangu kocha Charles Mkwasa alipokabidhiwa majukumu baada ya uongozi wa timu hiyo kulivunja benchi lote la ufundi
Mkwasa alitangazwa kuwa kocha wa muda kuanzia Novemba 05 mwaka huu baada ya Zahera pamoja na benchi lake lote la ufundi kuondolewa
Kocha huyo wa zamani wa timu ya Taifa, aliipokea Yanga ikiwa na changamoto nyingi, alilazimika kubadilisha mambo kadhaa ambayo yanaonekana kuisaidia timu hiyo
Mabadiliko hasa ya mfumo wa uchezaji yameifanya Yanga ifunguke zaidi na kutengeneza nafasi nyingi
Timu sasa haitegemei sana kufunga mabao yake kupitia mipira iliyokufa au kona
Katika michezo miwili iliyopita, Yanga imefunga mabao manne kawaida na mabao mawili kupitia mipira ya adhabu
Mkwasa anaonekana kujenga 'combination' mpya ya washambuliaji akitumia pacha ya Juma Balinya na David Molinga
Katika mchezo dhidi ya JKT Tanzania, Balinya na Molinga walianza pamoja ambapo wote walifanikiwa kufunga mabao kabla ya Molinga kutolewa kipindi cha pili
Wawili hao wamekuwa wakicheza pamoja hata mazoezini ikiwa ni ishara kuwa Mkwasa amewaamini na kuwapa jukumu la kuifungia timu hiyo mabao
Mshambuliaji Sadney Urikhob raia wa Namibia yeye hakujumishwa kabisa kwenye kikosi kilichoikabili JKT Tanzania
Huenda akabadilishiwa majukumu na kuanza kutumika akitokea pembeni badala ya mshambuliaji wa kati kama ilivyokuwa wakati wa Zahera



0 Comments