Windows

Kitambi, Adel waondoka Simba

Kitambi- Adel- waondoka -Simba-kocha -mkuu -Patrick -Aussems-uongozi -Adel-zrane-UEFA-
Mafunzo hayo ambayo Kitambi atahudhuria ni mafunzo ya ukufunzi wa makocha ambayo yatasimamia na UEFA na wataalamu wake watakaotoa mafunzo hayo watatoka Ulaya na watawasili nchini Desemba Mosi.

KIKOSI cha Simba kwa sasa kinaongozwa na kocha msaidizi Denis Kitambi na Adel Zrane tangu kocha mkuu Patrick Aussems aliposimamishwa na uongozi wa timu hiyo.
MCL Digital linafahamu Kitambi ambaye ndio anasimamia masuala yote ya kiufundi ndani ya timu hiyo kwa sasa ataondoka kuanzia Desemba 2 mpaka 10 mwaka huu atakwen

da kwenye mafunzo.
Mafunzo hayo ambayo Kitambi atahudhuria ni mafunzo ya ukufunzi wa makocha ambayo yatasimamia na UEFA na wataalamu wake watakaotoa mafunzo hayo watatoka Ulaya na watawasili nchini Desemba Mosi.

Wakati huo huo, Zrane naye ameomba ruhusu kwa mabosi wake ili kwenda kushughulikia mambo yake ya kifamilia kwa muda wa siku 10.
Kwa maana hiyo kikosi cha Simba huenda kitasimamiwa na mchezaji wa zamani na kocha wa Simba Queens, Mussa Hassan 'Mgosi'.

Kitambi alisema aliwasilisha barua kwa viongozi wake juu ya ruhusa ya kwenda kwenye mafunzo hayo ambayo yatachukuwa muda wa siku nane.
"Ngumu kupata nafasi kama hizi na mafunzo ndio maana niliomba uongozi wangu kunipa nafasi hiyo naamini wamekubaliana nami," alisema.

"Nimepokea barua kutoka Shirikisho la Soka nchini (TFF) ya kwenda kwenye mafunzo hayo ambayo nimekubaliana nao," alisema Kitambi.

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu, alisema kocha ambaye atakuja kuongoza timu hiyo ni suala la kusubiri muda muafaka kufika wataeleza kila kitu.
"Taarifa za Kitambi kwenda kwenye mafunzo pamoja na Adel kwenda kumaliza mambo fulani ya kifamilia hizo ninazo kwa maana hiyo ambaye atakuja hapa kuongoza timu ni suala la muda tu kwani mwanzo wa mwezi ujao tutakuwa na kocha," alisema Rweyemamu.

Post a Comment

0 Comments