Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema michakato ya ujenzi wa viwanja inayoendelea inakutokana na mipango ambayo wamejiwekea kama klabu na sio kwamba wamefanya hivyo baada ya kuona watani zao Simba wamekamilisha ujenzi wa viwanja vyao Bunju
Aidha Mwakalebela amesema hata utaratibu wa kukamilisha miradi hiyo uko tofauti. Uwanja wa Yanga unajengwa na Wanayanga wenyewe wakati Simba wamejengewa na Mo
"Sisi hatushindani na Simba katika ujenzi wa uwanja wetu. Tunatekeleza mipango ambayo tumejiwekea," amesema
"Hata vipaumbele ni tofauti, Simba wamejengewa uwanja na Mohammed Dewji wakati klabu ya Yangai itajenga uwanja wake kwa nguvu za wanaYanga wenyewe"
Yanga imeanza mchakato wa kujenga viwanja vyake vitatu eneo la Kigamboni walilopewa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda
Wakati huo Yanga inaendelea na ukarabati wa uwanja wake wa Kaunda
Hata hivyo ukarabati wa uwanja wa Kaunda kwa sasa umesimama kupisha mradi wa Serikali wa kudhibiti mafuriko eneo la Jangwani
Mkuu wa mkoa wa Dar Mh Makonda amesema mradi huo ukikamilika, suala la mafuriko eneo la Jangwani itabaki kuwa historia
0 Comments