Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema baadhi ya nyota waliokuwa majeruhi wanaendelea na program maalum chini ya uangalizi wa wataalam
Kumekuwa na maswali mengi kuhusu beki Paulo Godfrey 'Boxer' ambaye yuko nje kwa zaidi ya miezi mitatu
Aidha upande wa Juma Mahadhi yeye amekuwa nje kwa zaidi ya mwaka mmoja akiuguza majeraha ya goti aliyopata kabla ya kuanza kwa msimu uliopita
"Boxer na Mahadhi wanaendelea na program za mazoezi maalum ambayo yanasimamiwa na wataalamu. Pengine kuanzia mwezi wa 12 wataanza kuonekana uwanjani," amesema
Katika hatua nyingine Bumbuli amesema tetesi zinazowahusu baadhi ya nyota wao bado hazina uthibitisho hivyo ni vyema jambo hilo likazungumzwa wakati muafaka
"Ni vyema wanahabari mkawa wavumilivu kusubiri wakati muafaka kuandika baadhi ya mambo, amesema"
"Kuandika kuwa mchezaji fulani ataachwa wakati bado yuko kikosini kunashusha morali"
"Wakati utafika kila kitu kitawekwa hadharani"
Kalengo kurejea Dar kuendelea na matibabu
Mshambuliaji wa Yanga Maybin Kalengo atarejea nchini kuendelea na matibabu Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
Bumbuli amesema mshambuliaji huyo kutoka nchini Zambia anatakiwa kufika Hospitalini hapo Disemba 04
"Tayari tumeshamtumia tiketi ya Ndege arudi aje aendelee na matibabu" amesema
0 Comments