Windows

Balama kuikosa Alliance Fc




Kiungo Mapinduzi Balama hatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachosafiri kesho Jumatano kuelekea mkoani Mwanza kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Alliance Fc ambao utapigwa Ijumaa, Novemba 29

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema kiungo huyo hajapona majeraha ya nyonga aliyopata kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania siku ya Ijumaa

"Balama ameshindwa kufanya mazoezi kutokana na maumivu aliyopata kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania"

"Tutamuacha jijini Dar es salaam kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa majeraha yanayomsumbua," amesema

Balama atakosa mchezo huo dhidi ya waajiri wake wa zamani, klabu ya Alliance Fc

Kwenye mchezo huo Yanga pia huenda ikawakosa viungo wake watatu Feisal Salum, Mohammed Issa 'Banka' na Abdulaziz Makame ambao walirejea Zanzibar kujiunga na timu ya Taifa kuelekea michuano ya Chalenji itakayofanyika nchini Uganda kuanzia Disemba 07

Post a Comment

0 Comments