Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amevunja ukimya kufuatia sintofahamu inayoendelea kuhusu ajira yake
Kocha huyo amekiri kupokea ujumbe mwingi kutoka kwa mashabiki na wadau wa klabu ya Simba wanaotaka kufahamu nini kinaendelea
"Kwanza nawashukuru mashabiki kwa ujumbe na uungwaji mkono mnaoendelea kunionyesha," Aussems ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram
"Kwa sasa siruhusiwi kufanya kazi kwa kuwa bado nimesimamishwa na Bodi ya klabu ya Simba"
"Shauku yangu ni kuendelea kuwapa furaha nyinyi mashabiki wa Simba kwa soka zuri la kuvutia na kushinda mataji"
"Najua kila mmoja ana shauku hiyo.."
Aussems jana alifikishwa mbele ya Kamati ya Nidhamu kujibu tuhuma mbalimbali zinazomkabili
Leo Bodi ya Wakurugenzi inatarajiwa kukutana kupokea ripoti ya Kamati ya Nidhamu pamoja na kufanya uamuzi
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.
0 Comments