Windows

Ukifoji Tiketi Yanga Vs Pyramids Utakiona Cha Moto!

MAANDALIZI ya mchezo wa Yanga dhidi ya Pyramids yameendelea na mamlaka husika za mchezo huo zimeeleza kuwa tiketi zinatarajiwa kuanza kuuzwa leo Ijumaa zikiwa na alama maalum za utambuzi.

 

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, amesema tiketi za mchezo huo zitauzwa katika vituo 10 maeneo mbalimbali ya Mwanza na yeyote ambaye atakamatwa akihusika kutengeneza au kutumia tiketi bandia, atachukuliwa hatua kali kwa kuwa kuna micha-kato maalum inafanyika.

 

Yanga na wapinzani wao hao wa Misri wanatarajiwa kukipiga katika mchezo wa kuwania kufuzu Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika. Mchezo wa kwanza ni keshokutwa Jumapili kisha marudio yatafanyika wiki moja baadaye.

 

“Tiketi zitauzwa katika vituo vya Nyamagana uwanjani, Nyegezi Stand, Buzuruga Bus Stand, Shule ya Msingi Buhongwa, Lenana Hotel, CCM Kirumba, Buswelu Center, Igoma Stand, Posta Pamba Road pamoja na Mkolani.

 

“Tiketi zote zitakuwa na alama maalumu ya utambuzi ambayo itatufanya tuitambue tiketi halisi kwa urahisi zaidi,” alisema na kuongeza:

“Tumeamua kuuza hizi tiketi kwa kutumia moja ya makampuni makubwa hapa nchini na endapo mtu akibainika anadurufu tiketi lazima tumshughulikie kwa kuwa atakuwa anaihujumu timu yetu na hatutakuwa na huruma, tumedhamiria kufanya kazi zetu kwa weledi mkubwa.”

 

Aliongeza kuwa mashabiki wanatakiwa kununua tiketi mapema ili kukwepa usumbufu wakati wa kuingia uwanjani siku ya mchezo.

Stori na Johnson James

The post Ukifoji Tiketi Yanga Vs Pyramids Utakiona Cha Moto! appeared first on Global Publishers.


Post a Comment

0 Comments