

Aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Swedy Mkwabi.
KAMATI ya Uchaguzi ya Klabu ya Simba imesema tayari imepokea barua kutoka kwa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo kwa ajili ya kuandaa mchakato wa uchaguzi kujaza nafasi ya aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Swedy Mkwabi aliyejiuzulu hivi karibuni.
Nafasi ya mwenyekiti ndani ya Simba kwa sasa ipo wazi baada ya aliyekuwa anashika nafasi hiyo, Mkwabi kujiuzulu mwezi uliopita.
Simba italazimika kufanya uchaguzi wake Desemba ili kujaza nafasi hiyo ambayo kwa sasa ipo wazi na katiba inaelezea kuwa zoezi hilo lifanyike ndani ya siku 90 ambazo ni sawa na miezi mitatu.
Katibu wa kamati ya uchaguzi, Stephen Ally, amesema wao kama kamati tayari wamepokea barua kutoka kwa bodi ya wakurugenzi.
“Tayari tumepata barua kutoka kwa bodi ya wakurugenzi tunaifanyia kazi na hatua ambayo inafuata au kitu gani kitaendelea baada ya hapo kama kamati tutaweka wazi nini kinaendelea,” alisema Ally.
Mkwabi ambaye aliachia madaraka ndani ya Simba alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo katika uchaguzi mkuu uliofanyika Novemba 4, mwaka jana hivyo kuwa miongoni mwa wakurugenzi wa bodi ya Simba chini ya Mwekezaji Mohamed Dewji ‘Mo’.
The post Uchaguzi Simba Mambo Ni Moto appeared first on Global Publishers.



0 Comments