

Pamoja na kuwa na viungo wazuri, Yanga imekosa mtu mmoja muhimu wa kurahisisha maisha pale kwenye safu ya ushambuliaji
Msimu ulipita Yanga ilinufaika sana na ubunifu wa Ibrahim Ajib ambaye kocha Mwinyi Zahera alimtumia kwa jukumu maalum la kutengeneza mabao
Kwenye kikosi cha Yanga cha sasa jukumu la kuchezesha timu limeachwa kwa Feisal Salum 'Fei Toto'
Pamoja na ubora wake, Fei Toto bado sio mzuri kwenye kupiga pasi za mwisho, amekuwa akiifanya kazi vyema katikati ya dimba
Abdulaziz Makame ni kiungo mkabaji wakati Mohammed Issa 'Banka' nae ni mzuri kwenye kumiliki mpira na kuchezesha timu, lakini sio fundi wa kupiga mipira yenye madhara langoni kwa wapinzani
Nahodha Papy Tshishimbi nae kwa asili ni kiungo mkabaji ingawa wakati mwingine Zahera anamtumia kama kiungo mshambuliaji kutokana na changamoto za uhaba wa mabao zilizoikabili Yanga karibuni
Mapinduzi Balama anaweza akajaribiwa ingawa bado Zahera hajaamua kumtumia katika nafasi ya kiungo
Wakati alipokuwa Alliance Fc alikuwa akicheza nafasi hiyo
Yanga inahitaji kiungo aina ya Haruna Niyonzima ambaye atakuwa huru kufanya kazi ya kutengeneza nafasi
Niyonzima alikuwa tayari kurejea Yanga baada ya kuachana na Simba hata hivyo changamoto kubwa ikawa makubaliano ya mshahara na masuala binafsi
Niyonzima amerejea kwao Rwanda akiwa amejiunga na AS Kigali huko akipewa jukumu la unahodha wa timu hiyo
Lakini huyu ni mchezaji aliyecheza muda mrefu Yanga, anaweza kurejea wakati wowote kama viongozi watamuhitaji




0 Comments