

Septemba 28 ilikuwa siku mbaya sana kwa kiungo Abdulaziz Makame 'Bui' ambaye goli alilojifunga nchini Zambia lilipelekea Yanga kuchapwa mabao 2-1 na Zesco na kupelekea kuondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Katika michezo miwili aliyocheza kwenye ligi, Bui amekuwa mchezaji anayejituma zaidi kwenye kikosi cha Yanga
Timu inaposhambulia anaongeza nguvu na timu inaposhambuliwa yuko katika ulinzi
Leo juhudi zake zimezaa natunda kwani amemaliza machungu ya nchini Zambia baada ya kuifungia Yanga bao muhimu lililowahakikishia mabingwa hao wa kihistoria ushindi wao wa kwanza msimu huu
Bui ametoa zawadi bao hilo kwa mashabiki wote ambao wameendelea kumuunga mkono na kusahau tukio la Zambia



0 Comments