Mkurugenzi wa taasisi Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson na Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Philip Redman, wakibadilishana mawazo Katika hafla hiyo
Mkurugenzi wa Taasisi Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Philip Redman Katika hafla ya kukabidhi printer 9 iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa taasisi Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson (katikati) akiangalia Printers zilizotolewa kwa Taasisi hiyo na TBL, (Kulia)ni Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Philip Redman.
***
Kampuni ya TBL Group chini ya kampuni mama ya ABInBEV, imetoa msaada wa Printer 9, kwa taasisi ya Tulia Trust, ikiwa ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na taasisi hiyo kukabiliana na changamoto mbalimbali za kijamii hususani katika kuboresha sekta ya elimu nchini.
Hafla ya kukabidhi msaada msaada huo ilifanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Mkurugenzi wa Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson, Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Philip Redman ,na baadhi ya wafanyakazi kutoka taasisi hizo.
Akiongea katika hafla hiyo,Dk.Tulia, alishukuru kampuni ya TBL kwa jitihada ambazo imekuwa ikifanya kusaidia kukabiliana na changamoto za kijamii.
Akiongelea msaada huo, Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL, Irene Mutiganzi, alisema kuwa kampuni hiyo itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali na taasisi nyingine za maendeleo kushirikiana kupambana na changamoto mbalimbali kwenye jamii, hususani katika sekta ya elimu kama ambavyo inaendelea kutoa msaada wa Printer na vifaa vya kurahisisha elimu mashuleni.
0 Comments