CHIRWAKOCHA Mkuu wa Azam FC, Etienne Ndayiragije amemtaka mshambuliaji wake, Obrey Chirwa, kuhakikisha anafunga mabao mawili katika mchezo wao wa leo dhidi ya Triangle FC ukiwa ni wa Kombe la Shirikisho.
Mechi hiyo itapigwa nyumbani kwa Triangle nchini Zimbabwe huku wenyeji wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 walioupata kwenye mechi ya kwanza hivyo Azam sasa wanahitaji ushindi wa mabao 2-0 ili watinge hatua inayofuata.
Ndayiragije alisema kuwa, amempa Chirwa jukumu la kufunga mabao kwa kuwa mchezaji huyo anaweza kufanya hivyo kutokana na uwezo wake mkubwa wa kupambana na mabeki.
“Nilizungumza na Chirwa na nikamwambia kuwa anatakiwa kufunga mabao mawili ya haraka zaidi ili tuweze kupata ushindi katika mchezo huu, kwa sababu nguvu na uwezo wa kupambana na mabeki wa Triangle anao, kama akiamua kujitolea zaidi basi hiyo itakuwa kazi ndogo sana kwake,” alisema Ndayiragije.
Issa Liponda, Dar es Salaam
The post Chirwa akabidhiwa jukumu zito Azam appeared first on Global Publishers.
0 Comments