Azam inafanya mazoezi na kucheza mechi za kirafiki kujianda na mchezo wake wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Triangle United ya Zimbabwe utakaochezwa Septemba 15, jijini Dar es Salaam.
Kocha msaidizi wa Azam, Idd Cheche alisema tupo makini na lengo letu ni kufanya vizuri katika mashindano haya, kama ilivyo mechi yetu tutaanzia nyumbani na lengo letu ni kumaliza kabisa hapa tutakapokwenda Zimbabwe iwe kukamilisha ratiba tu.
Cheche alisema hilo linawezekana na ndio maana wamefanya maandalizi hayo makubwa kama kucheza mechi za kirafiki.
Akizungumzia wachezaji wao, Chirwa na Abalora kocha huyo alisema, walikuwa na maumivu madogo na wanawategemea uwanjani hivi karibuni: "Nafikiri kesho tunaweza kuwa nao ni maumivu madogo tu."
Azam imefuzu kwa hatua hiyo baada ya kuing'oa Fasil Kenema ya Ethiopia kwa jumla ya mabao 3-2, wakati Triangle ikiwaondosha Lukinzo kwa jumla ya mabao 5-0.
0 Comments