Windows

Zahera ajipange, uvumilivu wa Wanayanga utafika mwisho



Yanga imeanza kwa kipigo ligi kuu ya Tanzania Bara jana baada ya kufungwa bao 1-0 na Ruvu Shooting katika mchezo uliopigwa uwanja wa Uhuru

Ni matokeo yaliyowashtua mashabiki wa timu hiyo hasa ikizingatiwa mwishoni mwa wiki wametoka Botswana kuwalaza Township Rollers kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa

Aidha matokeo hayo pia yatazifanya mechi nyingine zote zinazofuatia kuwa ngumu zaidi kwa Yanga kwani ushindi huo wa Ruvu Shooting utaziongezea kujiamini timu hizo kuwa zinaweza kupata ushindi dhidi ya Yanga

Lakini pia kipigo hicho ni ujumbe kwa kocha Mwinyi Zahera kuwa anapaswa kujipanga kwelikweli ili kuweza kufanya vizuri msimu huu

Ni wazi msimu huu ushindani utakuwa mkubwa sana kwani ukiachana na vita ya kuwania ubingwa, timu nne zitashuka daraja moja kwa moja

Baada ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya ZESCO, Yanga itasafiri kwenda mkoani Mbeya kuzikabili Mbeya City na Tanzania Prisons kisha kuelekea Zambia

Kwa miaka mingi, uwanja wa Sokoine ni moja ya viwanja vigumu sana kupata matokeo kwa Yanga

Msimu uliopita Zahera alifanikiwa kuondoka na alama zote sita, lakini kwa mwenendo huu wa Yanga je msimu huu ataweza?

Kipigo cha jana kimemuongezea presha ya kupata matokeo Mbeya

Kwani kama hatapata matokeo ni dhahiri siku zake Yanga zitaanza kuhesabika

Licha ya uongozi wa Yanga kusisitiza kuwa kibarua chake kiko salama, lakini kwa mwenendo huu, lolote linaweza kutokea

Post a Comment

0 Comments