Windows

Wakazi wa Sangara-Babati wapata mradi wa Kisasa wa maji usiohitaji mhudumu


Na John Walter, Babati-Manyara

Zaidi ya wakazi 4000 wa kijiji cha Sangara kata ya Riroda wilaya ya Babati mkoani Manyara kunufaika na mradi wa maji safi na usafi wa Mazingira uliofadhiliwa na taasisi za Water Aid,Habitat For Humanit,UTT na e-Water kwa shilingi Milini 229.4.

Wakizunguza na Muungwana Blog  baada ya mradi huo kuzinduliwa, baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wamewashukuru wafadhili na Serikali kwa kuwapatia mradi huo wa maji kwani awali walikuwa wakiyapata maji hayo kwa shida na kwa umbali mrefu.

Hata hivyo wanaoishi maeneo yenye miinuko ambayo hayajafikiwa na Miundombinu ya maji wanasema bado tatizo hilo linaendelea kuwakabili kwani  mwendo bado ni ule ule kuyafuata yalipo hivyo serikali sasa iangalie namna ya kuwasaidia.

Akizindua mradi huo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Manyara, Mkuu wa wilaya ya Babati Elizabeth Kitundu amewataka wanakijiji hao wautunze mradi huo ili  uendelee kutumiwa na vizazi vijavyo.

Mradi huo ulikusudiwa kuwafikia wanakijiji wote wa Sangara kwa shilingi Milioni 776.8 lakini kutokana na upatikanaji wa fedha wamefanikiwa kuwafikishia wananchi 650 kwa awamu ya kwanza ambapo imetumika jumla ya  shilingi Milioni  229.4 za Kitanzania.

Akizindua mradi huo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Manyara, Mkuu wa wilaya ya Babati Elizabeth Kitundu amewataka wanakijiji hao wautunze mradi huo ili  uendelee kutumiwa na vizazi vijavyo kwani maji ni uhai wa kila kiumbe.

Dc Kitundu amesema kwamba kupatikana kwa mradi huo katika kijiji cha Sangara kumepunguza idadi ya watu ambao hawakuwa na huduma ya maji kabisa.

Amesema maeneo mengi hayana vyanzo  vya maji vya uhakika lakini kwa jitihada za wafadhili wamefanikiwa kuchimba kisima chenye urefu wa mita 120 chini ya ardhi na kupata lita 14,800 kwa saa hatua ambayo imeleta faraja kwa wakazi 650 wa vitongoji viwili vilivypopo maeneo yaliyofikiwa na miundo mbinu ya usambazaji.

Amesema mikakati  ya kuongeza mtandao wa maji kwa sehemu iliyobakia imeandaliwa na serikali kupitia Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) huku akiwaomba washirika walioshiriki katika awamu iliyokamilika pamoja na wadau wengine kuwaunga mkono ili kufanikisha jitihada hizo kwa wakati.

Nalo shirika la Wate Aid kupitia kwa Mkurugenzi wake hapa nchini  Abel Dugala, amesema Changamoto iliyopo kwa sasa ni usahihi wa Takwimu za hali ya maji nchini zinazotolewa hali inayopelekea wahisani kutoa fedha ndogo wakiamini kuwa maji yanapatikana

Amesema ni muhimu serikali ikaja na mfumo wa kuhakisha kuwa Takwimu za upatikanaji wa maji zinatunzwa na zinapatikana wakati wote.

“Kwa  hiyo amesema mradi wetu  unasisitiza ni kwa kiasi gani sekta binafsi ni muhimu katika kuhakikisha kwamba kuna uendelevu wa miradi yetu,kuhakikisha kwamba wote tunashiriki ili kufika pale tulipokusudia kufika ”alisisitiza Dugala

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika linaloshughilika na Makazi bora (HUMAN FOR HABITATY) Sailas Wachuku amewataka wananchi watakaonufaika na mradi huo ,kuyatumia maji hayo katika kuboresha makazi yao kwa kufanya ujenzi wa kisasa.

Wachuku amesema matarajio yao nikuona  mradio huo kwa awamu ya pili unakamilika haraka na kuwafikia wanakijiji  wote wa Sangara.

Naye mbunge wa jimbo la Babati vijijini Mheshimiwa Jituson amesema mfumo unaotumika katika malipo e-Water paid utasaidia kupunguza upotevu wa maji na kukukusanya mapato mengi yatakayosaidia kuanzisha miradi mingine ya maji,hivo  Halmashauri  ifanya mpango wa kuunganisha mfumo huo kwa watumiaji wote wa huduma ya maji.

Diwani wa kata ya Riroda (CCM) Charles Qwaray Muhale amesema ni furaha kubwa kwa wanakijiji wa Sangara chenye vitongoji vinne vya Sangara,Riroda,Endaberg na Hewas kwani adha ya maji ni ya muda mrefu eneo hilo lenye wakazi zaidi ya 4,000.

Hata hivyo katika wilaya ya Babati hali ya upatikanaji wa maji ni asilimia 71 tu kwani asilimia 29 ya wananchi hawana maji kabisa,kwaa maana kwamba kati ya vijiji 102 vya wilaya hii bado vijiji 24 havina huduma hiyo ambayo ni muhimu kwa kila Kiumbe na mimea.

Mfumo unaotumika katika kuwahudumia wanakijiji hao kupata maji ni wa kisasa ambao hauhitaji mhudumu bali mchota maji anachotakiwa ni kuwa na kadi yakle maalum inayomruhusu kufungua koki na kuchota maji wakati wote anapohitaji.

Post a Comment

0 Comments