Windows

Ukileta Umachepele na Simu Yako, Walahi Unaachika!

TUNAKUTANA tena kupitia safu hii nikiamini kwamba umzima na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku kama kawaida. Mimi niko poa kabisa tayari kukuletea mada ambayo inamgusa kila mtu aliye katika uhusiano.  Hakuna anayeweza kubisha kwamba tangu kumekuwepo na hizi simu za mkononi ndoa nyingi zimevunjika, wapenzi wengi wameachana na  wangine wakiendelea kuwa katika uhusiano lakini kwenye mazingira yasiyoridhisha. Wanandoa, wapenzi hawaelewani, hawaaminiani kutokana na simu za mkononi.

Mnapokuwa katika uhusiano kisha kufikia hatua ya kutoaminiana kisa simu, ni hatari sana. Yawezekana nyendo zako ndizo zinamfanya afikirie hivyo licha ya kwamba wanaume wengine wanakuwa na wivu wa kijinga. Yaani wao kila wakati wanawashutumu wapenzi wao kuwa na uhusiano wa kimapenzi na watu wengine hata kama hawana uhakika na kile wanachokisema. Kwa mtizamo wangu sioni sababu ya kuchungana kwa njia ya simu. Kitendo cha kudhani mpenzi wako anatumia simu yake kuwasiliana na mahawara inaonesha hakuna uaminifu kati yenu.

Wapo wanandoa ambao wamekuwa na kasumba ya kuchukuliana simu kwa siri na kuchunguza simu na sms zilizoingia. Wakikutana na sms tata, hukunikisha. Kwa nini kuwekana presha juu juu kiasi hicho? Unadhani kwa kufanya hivyo utakuwa umemdhibiti mwenza wako kutokukusaliti? Naamini huo sio ustaarabu na sio mfumo mzuri wa maisha.

Huwezi kumchunga mwenza wako kwa kupitia simu yake. Fahamu akiamua kukusaliti anaweza kufanya hivyo bila hata kuhusisha simu yake. Kikubwa ambacho kimekuwa kikichangia katika hili ni wivu, wivu ambao naamini kabisa hauna lengo la kujenga bali kubomoa. Nasema una lengo la kubomoa kwa sababu, ukichunguza sana utakuta wapenzi na wanandoa wengi ambao hawana uhuru na simu zao wamekuwa wakizozana mara kwa mara.

Wamekuwa wakipeana shutuma zisizo na ukweli na matokeo yake kuishi katika mazingira ya kuwindana. Katika hili naomba nikushauri kitu kimoja, kama unataka kutompa mpenzi wako mazingira ya kudhani unamsaliti kupitia simu yako, jiamini na punguza umachepele na simu yako!

Unapokuwa naye wala usioneshe kujishtukia. Wapo ambao kila wanapokuwa na wapenzi wao, wakipata sms tu, watajificha ili wasome fasta kisha wa-’delete’. Wakipigiwa kama hamjui anayempigia basi atakwenda kupokelea simu chooni na wengine huzima simu zao wanapokuwa na wapenzi wao.

Hivi unapofanya hivyo unataka mpenzi wako akufikirieje? Utamjengea mazingira gani ili akuamini sio kwamba kuna mshikaji mwingine uko naye kimapenzi kwa siri? Kimsingi kutokujiamini kwako kunaweza kukuharibia, ndiyo maana nasema kama kweli unampenda huyo uliye naye usiweke mazingira ya usiri kwenye simu yako. Wakati mwingine kuwa tayari kumjibu pale atakapokuuliza ni nani aliyekupigia simu au ujumbe huo unatoka kwa nani. Sio kila mara atakuuliza lakini pale atakapokuuliza mjibu

The post Ukileta Umachepele na Simu Yako, Walahi Unaachika! appeared first on Global Publishers.


Post a Comment

0 Comments