Windows

Ubora wa Simba unainua kiwango cha soka Tanzania



Mwekezaji wa klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewj 'Mo' amesema anaamini uwekezaji mkubwa anaofanya katika klabu hiyo, utasaidia kuinua kiwango cha soka nchini

Tangu aanze kuwekeza Simba misimu miwili iliyopita, Mo amefanikiwa kuifanya klabu hiyo kuwa klabu bora ukanda wa Afrika Mashariki na kati

Msimu uliopita Simba ilifanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, ikifanya hivyo baada ya miaka 15 tangu mara ya mwihso ifike hatua hiyo

Mo amesema mafanikio haya sio kwa Simba tu, bali ni kwa soka la Tanzania kwa ujumla

"Ukiiboresha Simba, utaiboresha Yanga na timu nyingine zote hapa Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki"

"Ninaamini Simba haiwajengi tu wapinzani, pia inazipa ujasiri timu zingine, ukiwa na timu nzuri za ndani pia unakuwa na timu nzuri ya Taifa na hapo ndio wachezaji wataweza kwenda kucheza Ulaya na sehemu nyingine," amesema Mo kwenye mahojiano na BBC


Mo amesema baadhi ya timu zimependezwa na aina ya mfumo wanaoutumia na zingependa kujifunza kutoka kwao

Mo anamiliki hisa asilimia 49 katika klabu ya Simba

Ndiye mwekezaji Mkuu na chachu ya mafanikio ya mabingwa hao wa Tanzania Bara kwa misimu miwili mfululizo

Post a Comment

0 Comments