Beki kisiki wa Yanga Kelvin Yondani amesema amerejea rasmi kikosini na atakuwepo kwenye mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers ambao utapigwa jiji la Gaborone nchini Botswana
Yondani, Juma Abdul na Andrew Vicent walikosa mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Taifa wakijiweka pembeni wakisubiri wakamilishiwe madai yao na uongozi wa Yanga
Kocha Mwinyi Zahera aliwaunga mkono wachezaji hao akiutaka uongozi umalizane nao ili warudi kikosini
Habari njema ni kuwa changamoto ya wachezaji hao imemalizwa na watakuwa sehemu ya kikosi kitakachoelekea mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Rollers
"Mimi sina tatizo na uongozi, kila kitu kimerekebishwa hivyo nawaambia mashabiki wasiwe na hofu," amesema
"Nitakuwepo kambini Moshi na pengine mchezo wa marudiano Botswana nitacheza"
Kurejea kwa Yondani kikosini huenda kukamlazimu Zahera kukifanyia mabadiliko kikosi chake cha kwanza
Zahera amekuwa akiwatumia Ally Mtoni na Lamine Moro katika nafasi ya ulinzi wa kati
Anaweza kumpeleka Mtoni pembeni na kati wakacheza Moro na Yondani
Katika mchezo huo wa marudiano, pia Zahera atakuwa na nyota waliokosa mchezo wa kwanza kutokana na kuchelewa kuwasili kwa vibali vyao
Nyota hao ni Farouk Shikalo, Mustapha Suleyman na David Molinga
0 Comments