Windows

Straika mpya Yanga, mabeki wale washibe

STRAIKA mpya wa Yanga David Molinga ameanza rasmi kazi Jangwani na juzi aliingizwa dakika za jioni kabisa katika mechi ya kirafiki dhidi ya Kariobang Sharks ya Kenya kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi, lakini unaambiwa huo mwili wake mabeki wa timu pinzani wana kazi.
Kwa jinsi mwili wake ulivyo na uwezo wake wa kucheza soka, ni lazima mabeki wa timu pinzani wale washibe la sivyo aibu itawapata kwani jamaa anatisha. Molinga aliyepewa jina la Falcao alianza kupiga mzigo rasmi na wenzake majuzi mazoezini ikiwa ni saa chache tangu asajiliwe kwa mkopo kutoka FC Renaissance du Congo, kabla ya juzi kupewa nafasi dakika tano za mwisho za pambano dhidi ya Sharks lililoisha kwa sare ya 1-1.
Kwenye mazoezi kwanza, raia huyo wa DR Congo alipotua Uwanja wa Uhuru mwili wake ukaacha gumzo kubwa akionekana kuwa kipande cha mtu na juzi ndiye aliyekuwa akijadiliwa zaidi na mashabiki wa timu hiyo katika Uwanja wa Taifa.
Hata kama akifanya mazoezi kisha akapungua, bado mshambuliaji huyo anatakiwa kuchungwa na mabeki kutokana na kuonekana kuwa na asili ya mwili wa nguvu na kwa dakika chache alizocheza dhidi ya Wakenya alithibitisha hilo, japo hakufunga.
Baada ya sekunde tano za Molinga, aligoma huku wenzake wakimpigia makofi wakitaka afanye, kitu, lakini jamaa alijikuta akinengua kimtindo na nyota wenzake kushangiliwa tukio lililowafanya Zahera na wasaidizi wake kuangua vicheko.
Straika huyo aliyemaliza msimu uliopita akiwa na mabao 11 huko DR Congo, amekuwa akifanya mazoezi peke yake kwa vile amechelewa kujiunga na wenzake na hata juzi Kocha Zahera aliamua kumuingiza ili kumtambulisha, lakini kazi itaanza akiwa Unguja.
Yanga inaenda Zanzibar kwa kambi ya muda mfupi ambapo pia watacheza mechi mbili kabla ya kurejea Dar es Salam Ijumaa kuisubiri Township Rollers ya Botswana.

Post a Comment

0 Comments