Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amewataka watanzania kuwa na utaratibu wa kupanga familia kulingana na uchumi walionao.
Ameyasemayo jijini Dar es Salaam, baada ya kufungua mkutano wa wabunge kutoka bara la Asia na Afrika unahusu masuala ya idadi ya watu na maendeleo.
Akizungumza katika mkutano huo, Ndugai amesema kuwa wao kama bunge kazi yao kubwa ni kuishauri serikali katika sera mbalimbali ambazo zitasaidia katika kuhakikisha kunakuwa na idadi endelevu ya watu ambao wanaishi maisha marefu na pia yenye uchumi mzuri.
“Kuna baadhi ya nchi zilizoendelea sana kama Japani na kwingine ambako idadi ya watu sehemu kubwa ni wazee inategemewa idadi yao kupungua”.
“Uwe na idadi ya watu kuendana na uchumi wetu katika kiwango cha familia, kaya na baadae katika taifa kwa ujumla,”amesema Ndugai.
0 Comments