

Kikosi cha Yanga leo kimeingia siku ya pili ya maandalizi yake kuelekea mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers
Yanga imejichimbia wilayani Moshi ikifanya mazoezi ya 'kufa mtu'
Uongozi wa Yanga umechagua kuweka kambi Moshi sababu hali ya hewa ya sasa ya eneo hilo inaendana na hali ya hewa ya Botswana
Mabingwa hao wa kihistoria wana siku tisa za kujiweka sawa kabla ya mchezo huo ambao utaamua timu itakayokwenda raundi ya kwanza
Hata hivyo Yanga itakuwa na kibarua cha kupata ushindi ugenini baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 nyumbani
Kocha Mwinyi Zahera amesema hana wasiwasi na kikosi chake, wataweza kupata matokeo ugenini



0 Comments