Nyota na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Mbwana Samatta atakutana uso kwa uso na mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Liverpool inayoongozwa na beki mshindi wa tuzo ya mchezaji bora Ulaya, Virgil Van Dijk kwenye mashindano hayo msimu ujao.
Hiyo ni kufuatia kitendo cha timu yake ya Genk kupangwa kundi E pamoja na mabingwa hao wa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mara sita katika droo ya upangaji wa makundi ya mashindano hayo msimu huu iliyofanyika leo huko Paris, Ufaransa.
Van Dijk anatajwa kama mmoja wa mabeki bora duniani kwa sasa ameshinda tuzo ya mchezaji bora Ulaya akiwashinda Messi na Ronaldo katika hafla hiyo.
Mbali na Van Dijk, Samatta pia atakumbana kwa mara nyingine na beki wa Senegal, Kalidou Koulibaly ambaye pia timu yake Napoli imeangukia kwenye kundi hilo.
Samatta na Koulibaly, walikutana kwenye Fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) mnamo Juni 23 katika mchezo wa kundi C ambao Senegal iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Liverpool, Napoli na Genk zote zimepangwa pamoja kwenye kundi E linalohusisha pia timu ya Salzburg kutoka Austria.
Katika uchezeshaji wa droo hiyo, timu 32 ziligawanywa kwenye vyungu vinne vyenye timu nane kila kimoja ambapo chungu cha kwanza kilihusisha timu zilizotwaa ubingwa kwenye nchi zao, bingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita na pia bingwa wa Europa League.
Chungu cha kwanza kilikuwa na timu za Liverpool, Chelsea, Barcelona, Manchester City, Juventus, Bayern Munich, Paris Saint-Germain na Zenit St Petersburg wakati kile cha pili kilikuwa na timu za Real Madrid, Atletico Madrid, Borussia Dortmund, Napoli, Shakhtar Donetsk, Tottenham Hotspur na Ajax, Benfica.
Kwa upande wa chungu cha tatu kilijumuisha timu za Olympique Lyon, Bayer Leverkusen, FC Salzburg, Olympiakos, Club Brugge, Valencia, Inter Milan na Dinamo Zagreb wakati timu za Lokomotiv Moscow, Genk, Galatasaray, RB Leipzig, Slavia Prague, Red Star Belgrade, Atalanta, Lille ziliwekwa kwenye chungu cha nne.
Kwa kupangwa kundi E, Samatta amekwepa kukutana na nyota wawili wanaotamba duniani kwa sasa, washambuliaji Cristiano Ronaldo wa Juventus na Lionel Messi wa Barcelona.
Ronaldo na Juventus yake wameangukia kwenye kundi D lenye timu za Atletico Madrid, Bayer Leverkusen na Lokomotiv Moscow wakati Barcelona yenyewe imepangwa kundi F na timu za Borussia Dortmund, Inter Milan na Slavia Praha.
Makundi
Kundi A: Paris Saint-Germain, Real Madrid, Club Brugge, Galatasaray
Kundi B - Bayern Munich, Tottenham, Olympiakos, Red Star
Kundi C - Man City, Shakhtar Donetsk, Dinamo Zagreb, Atalanta
Kundi D - Juventus, Atletico Madrid, Bayer Leverkusen, Lokomotiv Moscow
Kundi E - Liverpool, Napoli, Salzburg, Genk
Kundi F - Barcelona, Borussia Dortmund, Inter Milan, Slavia Prague
Kundi G - Zenit St. Petersburg, Benfica, Lyon, RB Leipzig
Kundi H - Chelsea, Ajax, Valencia, Lille

0 Comments