Windows

Rais wa nchi hii Afrika kusherekea miaka 40 madarakani


Rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Obiang Nguema anasherehekea miaka 40 madarakani wiki hii. Nguema, 77 anatajwa kumuandaa mtoto wake Teodorin 51 ambaye ni Makamu wake wa Rais wa sasa kuja kushika madaraka.

Teodoro Obiang aliingia madarakani August 3, 1979 baada ya yeye na viongozi wengine askari kumpindua aliyekua Rais wa wakati huo ambaye ni mjomba wake dikteta Fransisco Macias Nguema.

Equatorial Guinea, taifa lenye kutegemea uchumi wa mafuta ni moja kati ya mataifa yanayotajwa kukithiri kwa rushwa, Makamu wa Rais na Mtoto wa Rais aliteuliwa kushika wadhifa huo 2012 huku 2017 akihukumiwa na mahakama moja nchini Ufaransa kwa makosa ya kumiliki mali nyingi zilizopatikana kwa udanganyifu.

Post a Comment

0 Comments