Windows

Naibu Waziri wa Elimu aagiza watendaji wa idara ya uthibiti ubora wa shule


Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha ameagiza watendaji wa idara ya uthibiti ubora wa shule kusimamia kwa makini miradi ya ujenzi wa ofisi za Uthibiti ubora wa shule pamoja na fedha zinazotumwa kwa ajili ya ujenzi huo katika Halmashauri za wilaya mbalimbali nchini.

Naibu Waziri Ole Nasha amesema hayo mkoani Geita wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ya sekta ya Elimu inayotekelezwa mkoani humo, ambapo amesema serikali haitamvumilia mtumishi yeyote atakayehujumu ama kutumia vibaya fedha hizo zilizotolewa na wizara kwa ajili ya kujenga ofisi hizo.

Amesema miradi ya ujenzi wa ofisi hizo ni muhimu sana kwa wizara kwani ili kuwa na maendeleo katika sekta ya elimu lazima kuwa na uthibiti ubora wa shule ulio mahiri, wenye uwezo wa kukagua shule na wenye vitendea kazi vya kuwezesha wathibiti ubora wa shule kufanya kazi katika mazingira wezeshi.


Post a Comment

0 Comments