

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania ambaye kwa sasa anakipiga KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta leo ameacha swali kwa wadau na mashabiki soka nchini.
Ni muda mchache baada ya kumaliza mahojiano na kituo kimoja cha Radio nchini belgium GRK kuhusu maisha yake soka na mipango ya mbeleni.
"Nilikuwa na mahojiano mazuri leo na radio GRK, nikijibu maswali ya mashabiki mtandaoni, kuna swali niliulizwa, kati ya KRC Genk kuchukua kombe la Champion League au Tanzania kucheza World Cup kipi utachagua, unadhani nilichagua kipi?," ameuliza Samatta.




0 Comments