Mashabiki wenye hasira na ghadhabu wa Korea Kusini wanataka walipwe fidia baada ya Cristiano Ronaldo kushindwa kuingia uwanjani wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Juventus.
Ronaldo alikuwa amesaini mkataba wa kucheza dakika 45 dhidi ya timu ya Ligi K lakini alikaa kwenye benchi nje ya uwanja.
Mashabiki walijawa na ghadhabu na hata wakaanza kushangilia kwa kutaja jina la hasimu wake Lionel Messi.
0 Comments