Kontena kutoka China lililosafirishwa kuleta vifaa vya kielektroniki kwa ajili ya Bunge la Kenya, limefunguliwa na kukutwa tupu lilipofika Nairobi.
Ubalozi wa China nchini Kenya umesema umestushwa na tukio hilo ambapo tayari Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ameanza uchunguzi.
Ubalozi umesema unaaamini uchunguzi wa Polisi utasaidia kupatikana vifaa hivyo. Vifaa hivyo vilikuwa ni msaada kutoka China ambavyo iliahidi kulisaidia Bunge la Kenya
0 Comments