JACKSON Mayanja, Kocha Mkuu wa KCM amesema kuwa kinachowashinda wachezaji wake kwa sasa kupata matokeo ni kushindwa kutumia akili wakiwa uwanjani na badala yake wanatumia nguvu nyingi.
KMC ilianza kufungua pazia la ligi kwa kuambulia kichapo cha bao 1-0 mbele ya Azam FC mchezo uliochezwa uwanja wa Uhuru.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mayanja amesema kuwa kwa sasa mpira umebadilika hauhitaji kutumia nguvu nyingi bali akili pamoja na mbinu uwanjani.
“Wachezaji wangu wengi nimekuwa na kazi kubwa ya kuwafundisha namna ya kutumia akili na sio nguvu ndicho ambacho kinatuponza kushindwa kuwa na matokeo chanya kwenye mechi zetu za mashindano.
“Hilo limechangia mimi kufungwa na Azam FC pia nina lundo la majeruhi ambao mpaka sasa sijawatumia na ninalazimisha kuwatumia wachezaji ambao wanacheza nafasi wasizozijua kwa asilimia mia,” amesema Mayanja.
0 Comments