STAA wa zamani wa Arsenal, Ian Wright amemshangaa kocha Unai Emery kutumia fomesheni ya diamond kwenye mechi ya kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Liverpool wikiendi iliyopita, wakati alipaswa kutumia watu watatu kwenye safu ya ushambuliaji.
Kocha Emery aliamua kuanza na fomesheni ya 4-4-2 ambapo Pierre-Emerick Aubameyang na Nicolas Pepe, walianza kwenye fowadi na kuanza kutumia mfumo mwingine, ambao angewatumia washambuliaji watatu sasa na Alexandre Lacazette.
Mtindo wa uchezaji alioanza nao Emery kwenye mechi hiyo ya Anfield iliwafanya mabeki wa pembeni wa Liverpool, Trent Alexander Arnold na Andy Robertson kuwa na nafasi kubwa ya kupanda mbele na kuwafanya kushinda kirahisi kwa mabao la Joel Matip na Mohamed Salah, aliyefunga mara mbili.
Kocha Emery alimwingiza Lacazette wakati tayari timu ilikuwa imefungwa mabao matatu, huku bao lao la kujifariji lilifungwa na kiungo Lucas Torreira na hivyo kuondoka uwanjani hapo wakishindwa kuweka rekodi ya mwanzo mzuri wa msimu kwa asilimia 100.
Ian Wright aliamini Emery angeanza na Lacazette, Aubameyang na Pepe kwenye fowadi yake ili kuwafanya Liverpool kuwa bize kwenye kuwakaba kuliko kuwapa ahueni ya kuja mbele kushambulia.
"Kilickuwa kitu kimoja kilichonishangaza sana. Kabla ya mechi nilidhani Lacazette, Pepe na Aubameyang wangeenza, lakini haikuwa hivyo na Liverpool walifurahia kuona timu ilivyopangwa," alisema Ian Wright.

0 Comments