Windows

Abdul amerejea wakati muafaka



Nahodha Msaidizi wa Yanga Juma Abdul yuko mkoani Kilimanjaro na kikosi cha timu hiyo kinachojiandaa na mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers

Abdul hakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilichokuwa kimeweka kambi mkoani Morogoro kutokana na sintofahamu iliyojitokeza baina yake na uongozi

Hata hivyo mkongwe huyo ana karibu siku 10 za kujiimarisha tayari kubeba jukumu lake nchini Botswana

Yanga itamuhitaji Abdul kwenye mchezo huo kwani beki wake tegemeo Paulo Godfrey 'Boxer' aliyepata majeraha kwenye mchezo wa kwanza anaweza kukaa nje kwa zaidi ya wiki mbili

Post a Comment

0 Comments