Waziri wa Maji, Prof Makame Mbarawa amefungua mkutano wa saba wa Bodi za Maji za Mabonde unaofanyika Ujiji mkoani Kigoma na kuzindua taarifa ya faida na changamoto za ushirikiano na usimamizi wa rasimali za maji Shirikisho pamoja na taarifa za rasimali za maji.
Mkutano huo ni sehemu ya utaratibu wa Wizara ya Maji kufanya mikutano ya pamoja ya usimamizi wa rasimali za maji kila mwaka kwa kuwakutanisha wataalamu wa sekta ya maji ili kujadili na kuzitafutia ufumbuzi changamoto za sekta ya maji nchini na kikanda kwa Mabonde ambayo ni shirikishi.
Katika mkutano huo Prof Mbarawa amewataka wenyeviti na maafisa maji wa bodi za maji na mabonde kusimamia kikamilifu rasimali za maji kwa uadilifu, kudhibiti uchafuzi na kuhakikisha matumizi sahihi ya maji kwa ajili ya maendeleo ya jamii.
0 Comments