Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amelitaka Jeshi la Polisi kutowasumbua waendesha bodaboda kwa kuwakamata hovyo barabarani na bodaboda hizo kuzihifadhi vituo vya polisi huku wamiliki wa vyombo hivyo wakiteseka kuzipata.
Ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara alipokuwa anajibu maswali mbalimbali ya wananchi wa Mji Mdogo wa Kisorya, Kata ya Kisorya, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, jana.
“Bodaboda akifanya makosa mpigeni faini, na apewe muda wa siku saba kulipa faini hiyo kama inavyokua katika faini za magari," ameeleza Waziri Lugola.
Ameendelea kwa kusema, "Na nilishasema, bodaboda ambazo zinapaswa kuwepo kituoni ni za aina tatu tuu, ambazo zilizoshiriki uhalifu, zilizookotwa na zilizopata ajali, ndizo nilizoagiza ziwepo kituoni,”.
0 Comments