Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kingwangalla akizungumzia juu ya maoni ya watu kuhusu sanamu ya Baba wa Taifa aliyomkabidhi Rais Magufuli amesema kuwa "Jana kwa nia njema kabisa Wizara yetu iliamua kumpa tuzo maalum Rais Magufuli ambayo ina maneno aliyoyasema Mwl. Nyerere mwaka 1961, lakini nimeona imezua mjadala sana kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii jambo ambalo ni zuri imeweka alama”
Ameongeza kuwa “Hatuyapuuzi maneno na comment za Watanzania wenzetu ambayo yanahusiana na uumbaji wa lile sanamu,kama kuna mapungufu sisi ndio wenye dhamana ya kuangalia kama liko sahihi, Wataalamu tunao Serikalini tutawaita watuelekeze kama kuna mapungufu yatarekebishwa”
Aidha, amefafanua kuwa “Vijana na Wanasiasa wanaozungumza kwenye mitandao tunawashukuru kwa comment zao na tunawatoa wasiwasi kuwa tutalishughulikia, jambo ambalo limenifurahisha ni kwamba vijana bado wanaikumbuka taswira halisi ya Mwl.Nyerere,ni jambo kubwa sana kwetu kama Taifa.”
Lakini pia amesema “Nimefurahishwa pia na mjadala wa faru Rajabu ambaye pia yupo kwenye mikono salama ya TANAPA na anaendelea kufanya kazi yake vizuri kabisa bila shida, tutatafuta mtoto wake mmoja machachari tutamleta kwenye Hifadhi ya Burigi Chato"
0 Comments