Polisi wa Uturuki wamelazimika kutumia risasi za mpira kutawanya wanaharakati wa mapenzi ya jinsia moja ambao walikuwa wakiandamana katikati mwa mji wa Istanbul.
Kwa mara ya tano katika kipindi cha miaka mitano, Gavana wa Istanbul amekuwa akipiga marufuku maandamano hayo.
Hata hivyo licha ya marufuku huo, mamia ya wanaharakati wa mapenzi ya jinsia moja juzi walijumuika katika bustani ya Taksim kwa ajili ya maandamano hayo. Maandamano kama hayo yaliandaliwa mwaka wa 2014 na kuhudhuriwa na watu zaidi ya 100,000 kupinga uhasama na chuki dhidi ya wapenzi wa jinsia moja.
0 Comments