Windows

Jeshi la zima moto Njombe latinga Baraza la Madiwani


Na.Amiri kilagalila, Njombe

Wakati hofu ikianza kutanda kwa wananchi mbalimbali juu ya moto kichaa ambao huibuka na kushika kasi kuelekea msimu huu wa maandalizi ya mashamba jeshi la zima moto na uokoaji mkoa wa Njombe limelazimika kuingia kwenye vikao vya mabaraza ya madiwani kutoa elimu ya moto.

Katika kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Njombe mkaguzi msaidizi wa zima moto mkoa wa njombe (fire martial) Deogratius lyimo anasema kufika katika baraza la madiwani na kutoa elimu ya moto kutasaidia kufikisha ujumbe kwa wananchi kupitia madiwani huku akisema miongoni mwa sababu za kuzuka kwa moto katika maeneo mbalimbali ni kutokana na shughuli za kilimo,uchomaji mikaa pamoja na visasi vinavyotokana na migogoro ya ardhi.

Valentino Hongoli ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe ambaye amesema kuwa elimu hiyo imewafikia kwa muda mwafaka ikizingatiwa wanaelekea kwenye maandalizi ya mashamba huku akitaka kuendelea kuzingatiwa kwa sheria ndogondogo walizojiwekea za uandaaji mashamba.

Shaibu masasi ni diwani wa kata ya Matembwe na Lunyamadzo mhidze ni diwani wa kata ya Ukalawa wamekiri kuwapo kwa tatizo kubwa la uchomaji wa moto katika kata zao na kuwasababishia hasara kubwa wananchi huku wakitaka elimu hiyo iendelee kutolewa hadi kwa wananchi na kwenye taasisi za umma zilizopo katika maeneo yao ambako kuna mitungi ya zima moto.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Kidegembye Bwire majogoro nyagenge anasema kuwa kwa sasa tatizo la uchomaji moto hovyo limepungua baada ya sheria ndogondogo kusimamiwa ipasavyo licha ya elimu kutakiwa kuendelea kutolewa.

Mbali na kusababisha hasara kubwa kwa wananchi baada ya kuunguliwa kwa miti yao  na moto kichaa lakini pia husababisha athari katika mazingira na kusababisha kuwapo kwa mabadiliko makubwa ya tabia nchi.

Post a Comment

0 Comments