Windows

HESLB yaanza kupokea maombi ya mikopo


Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), leo inafungua dirisha la uombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2019/2020.

Bodi hiyo imeboresha utoaji elimu kwa waombaji wapya pamoja na kutembelea kambi za jeshi walizopo wanafunzi kuwapa maelekezo ya kujaza fomu kabla ya kurejea majumbani kuomba mikopo.

Aidha, mwaka huu, wamefanya maboresho katika muongozo wa utoaji mikopo kwa umri wa waombaji waliopo vyuoni kwa kuongeza umri mpaka miaka 35 badala ya 33 na wanaruhusiwa waliomaliza miaka mitano iliyopita na si miaka mitatu.

Ofisa Mawasiliano Mwandamizi wa bodi hiyo,Veneranda Malima amesema hayo katika banda la bodi hiyo kwenye viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam maarufu Sabasaba.

Alisema katika maonesho hayo wamesogeza huduma kwa jamii na wadau kwa kutoa taarifa za wanaorejesha mikopo, wanaotaka kujua salio na wanaotaka kulipa huku wanafunzi wanaotaka kufahamu kuhusu fedha zao za mafunzo ya vitendo watahudumiwa.

Malima alisema lengo la uboreshaji huo ni kutoa nafasi kwa wanufaika wengi kupata mikopo hasa kwa waliopata matatizo kama ya kufiwa na wazazi hivyo kuwa na uhitaji.



Post a Comment

0 Comments