Windows

DC Ngubiagai awatuliza na kuwapa somo wakulima wa ufuta


Na Ahmad Mmow-Kilwa

 Kufuatia malalamiko ya baadhi ya wakulima wa ufuta katika wilaya ya Kilwa, mkoani Lindi, kutokana na kupanda na kushuka kwa bei ya zao hilo. Mkuu wa wilaya hiyo, Christopher Ngubiagai amewaomba waridhie mabadiliko hayo ya bei.

 Ngubiagai ambae alitoa rai hiyo kufuatia malalamiko ya baadhi ya wakulima kutokana na kupanda na kushuka kwa bei ya ufuta katika msimu huu, alisema bei ya zao hilo inaamriwa na soko. Hali ambayo ni tofauti na misimu iliyopita, ambayo serikali ililiwekewa bei dira (bei elekezi).

 3; Alisema bei za mazao zinazoamriwa na soko zinaweza kupanda na kushuka, hivyo wakulima wanatakiwa kukubali mabadiliko hayo ambayo niya kawaida kwa mazao ambayo bei zake zinaamriwa na soko.

''Ndugu zangu na wananchi wangu thamani ya mazao ambayo bei zake zinaamriwa na soko zinaweza kupanda na kushuka, sio ajabu. Uzalishaji ukiwa mdogo kuliko mahitaji, bei inaweza kushuka. Lakini uzalishaji unapokuwa mdogo kuliko mahitaji ni lazima bei zitakuwa kubwa,'' alisema Ngubiagai.

Aidha mkuu huyo wa wilaya ya Kilwa alitoa wito kwa wakulima kusimamia na kudhibiti ubora wa zao hilo. Akibainisha kwamba

 Bei ya ufuta katika msimu huu imekuwa ikipanda na kushuka ambapo katika mnada wa kwanza, bei ya kilo moja ilifikia Tsh. 3,100. Hata hivyo zilishuka na kufika Tsh. 2,730.

Post a Comment

0 Comments