Taarifa ya Yanga kumuwania mshambuliaji wa zamani wa Simba Laudirt Mavugo, imesambaa sana kwenye mitandao ya kijamii
Inaelezwa tayari makubaliano yamefikiwa kumpa mshambuliaji huyo wa Napsa Stars ya Zambia mkataba wa miaka miwili
Hata hivyo Yanga imekanusha taarifa hiyo ikisisitiza mpaka sasa hakuna mchezaji aliyetangazwa kusajiliwa na Yanga zaidi ya Papi Tshishimbi
Afisa Habari Msaidizi wa Yanga Godlisten Anderson 'Chicharito' amesema wachezaji wengi wamekuwa wakihusishwa na Yanga kwa kuwa ni timu kubwa
"Wachezaji wengi wanahusishwa kujiunga na Yanga kwa kuwa hii ni timu kubwa, lakini pia huu ni wakati wa usajili tetesi kama hizo lazima ziwepo," amesema
"Hata hivyo Kamati Maalum iliyoachiwa jukumu la usajili na kocha Mwinyi Zahera bado haijatangaza wachezaji waliosajiliwa"
"Lakini pia kamati iliachiwa vigezo na sifa za wachezaji ambao wanatakiwa wasajiliwe, hivyo kama Mavugo anazo sifa hizo anaweza kuvaa uzi wa Yanga msimu ujao"
"Ifahamike mpaka sasa ni mchezaji mmoja tu Papi Tshishimbi ambaye amesajiliwa na Yanga baada ya kupewa mkataba mpya, wengine watatangazwa baada ya Kamati ya usajili kumaliza kazi yake"
Yanga bado haijaweka hadharani majina ya wachezaji waliosajiliwa lakini inafahamika wapo ambao tayari wamesaini mikataba ya kuwatumikia mabingwa hao wa kihistoria
Mavugo amekuwa na msimu mzuri nchini Zambia akiifungia Napsa Stars mabao 10 katika michezo 18 aliyocheza na kuibuka mmoja wa wafungaji bora wa 'Transitional League' ya Zambia
Mavugo amefungana na Adam Zikiru na Austin Muwowo wote wa Forrest Rangerscut
Mwezi uliopita kwenye moja ya michezo ya ligi, Mavugo alifunga hat-trik na kuisaidia timu yake kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Forrest Rangers ugenini
Hakupata mafanikio makubwa katika miaka miwili aliyoitumikia Simba lakini nchini Zambia ameonyesha uwezo mkubwa sana
Ameitwa kwenye kikosi cha awali cha timu ya Taifa ya Burundi kitakachoshiriki fainali za AFCON 2019 zitakazofanyika baadae mwezi huu nchini Misri
0 Comments