Windows

Waziri Mkuu, Dr. Mwakyembe Walivyotua Kwenye ‘Kubwa Kuliko’

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (wa pili kulia) akiwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni Dr. Harrison Mwakyembe (wa tatu kulia) sambamba na Mwenyekiti wa Yanga. Dr. Mshindo Msolla,  leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa leo amejiunga kwenye tamasha maalumu la kuichangia klabu ya  Yanga ambalo limefanyika ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam alipoongozana na Waziri wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni Dr. Harisson Mwakyembe.

Viongozi wengine ambao wamefika ni pamoja na rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete;  Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Anthony  Mavunde;  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda;  Mwigulu Nchemba, George Mkuchika na wengine kibao.

Mbunge wa Iramba, Mwigulu Nchemba (katikati) akitua ukumbini.

Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Dkt. Mshindo Msolla (kulia) akiongea jambo na aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati ya kuichangia Yanga na Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde.

Msanii wa filamu Bongo na mwanamitindo, Jacqueline Wolper (katikati) akiwa ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

PICHA NA MUSA MATEJA | GPL

The post Waziri Mkuu, Dr. Mwakyembe Walivyotua Kwenye ‘Kubwa Kuliko’ appeared first on Global Publishers.


Post a Comment

0 Comments