Windows

Waliopisha miradi ya umeme kulipwa, serikali yawataka kuwa na subira


Wananchi waliopisha miradi mikubwa ya umeme kwenye mikoa ya Pwani, Dar es Salaam na Dodoma watalipwa fidia wakati wowote baada ya uhakiki kukamilika.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu alipokuwa akizungumza na wananchi wa mtaa wa vitendo, alipokuwa akizindua uwashaji umeme.

Mgalu amesema, limechukua muda mrefu kutokana na uhakiki na fedha hizo zisingeweza kutolewa haraka, kwani wengine walikuwa wakitaka kujinufaisha kupitia malipo hayo.

"Tunaomba samahani kwa kuchelewesha fidia kwani tunajua baadhi wanasubiri tangu mwaka 2013 lakini kulihitajika umakini sana ili kuepuka upigaji," alisema Mgalu.

Alitaja maeneo hayo kuwa ni njia za Rufiji Chalinze, Dar es Salaam hadi Chalinze na Chalinze hadi Dodoma, ambapo wanatarajia kukutana na wananchi wanaohusika na jambo hilo.

"Wananchi waliopitiwa na miradi hiyo watalipwa hakuna atakayenyimwa haki yake kikubwa ni kuwa na subira tu kwani wajibu wa serikali kufanya hivyo," alisema Mgalu.

Aidha, alisema kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha miundombinu, inawafikia wananchi ili ibaki kupeleka umeme majumbani.



Post a Comment

0 Comments