Mashabiki wa burudani haswa wapenzi wa muziki wa singeli usiku wa kuamkia leo katika kusherehekea Siku Kuu ya Idd El Fitri walipata bonge la burudani kwenye Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar live katika onesho maalum la usikuwa uswazi ambalo lilikuwa noma saaana aisee.
Katika onesho hilo miamba wa singeli walionesha na umwamba katika mpambano huo ulianza kutimua vumbi baada ya kumalizika kwa michezo ya watoto.
Katika mtifuano huo aliayeanza kurusha mawe alikuwa Mfalme Ninja ambaye baada ya kuwalimisha vyakutosha mashabiki alimpisha jukwaa, Dullah Makabila.
Dullah Makabila wakati akiendelea kutafuta kabila la kuoa fungakazi ilikuwa kwa Sholo Mwamba ambaye aliwasugulisha gaga watoto wa uswazi mpaka majooo… Ama kweli Usiku wa Uswazi ulikuwa noma sana.
HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS/GPL
The post USIKU WA USWAZI DAR LIVE, IDDI EL FITRI ILIKUWA NOMA AISEE!!! (PICHA +VIDEO) appeared first on Global Publishers.
0 Comments