Windows

CAF Yafuta Matokeo ya Fainali Ligi ya Mabingwa

Shiikisho a Soka Barani Afrika (CAF) limeyafuta matokeo ya mechi ya fainali ya pili ya Mabingwa Barani Afrika yaliyoipa Ubingwa Esperance ya Tunisia dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco ambao waligoma kuendelea na mchezo huo kufuatia refa kukataa bao lao huku mfumo wa VAR ukishindwa kabisa kufanya kazi.

 

Mechi hiyo iliyopigwa usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita, itarudiwa baada ya mashindano ya AFCON katika uwanja huru huko Afrika Kusini, Juni 30 mwaka huu.

Washindi wameambiwa warejeshe kombe mara moja pamoja na medali.

 

Ndani ya miezi 6 fainali za klabu bingwa za America na Afrika zimeingia na dosari. (Shambulio la Boca Juniour na River Plate, mgomo wa Wydad vs Esp).

The post CAF Yafuta Matokeo ya Fainali Ligi ya Mabingwa appeared first on Global Publishers.


Post a Comment

0 Comments