Simba imetwaa ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara kwa misimu miwili mfululizo na kwa kikosi hikihiki kilichopo, inaweza kutwaa ubingwa huo tena msimu ujao
Hata hivyo baada ya kufika robo fainali ya ligi ya mabingwa msimu uliomalizika, Simba inaweza kufanya vizuri zaidi kwenye michuano hiyo
Kocha Patrick Aussems hivi karibuni alisaini mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuwafundisha mabingwa hao wa Tanzania Bara
Masharti aliyopewa kwenye mkataba huo mpya hayatofautiani sana na ya mkataba uliopita
Kutwaa ubingwa wa ligi kuu ni sharti la kwanza na la pili anapaswa kuipeleka Simba angalau hatua ya makundi huku lengo kuu likiwa kufika robo fainali
Hapo ndipo umuhimu wa kufanya usajili wa maana unapokuja
Udhaifu mkubwa wa Simba msimu uliomalizika katika michuano ya CAF ilikuwa michezo ya ugenini
Simba ilifunga bao moja tu ugenini na kuruhusu mabao 16, takwimu hizi zinadhihirisha Simba inahitaji maboresho makubwacut
Wachezaji wanaopaswa kusajiliwa na Simba kwa ajili ya michuano ya Kimataifa ni wale wenye uzoefu wa michuano hiyo lakini pia wenye uwezo wa hali ya juu
Kama alivyosema Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mohammed Dewji 'Mo', Simba inashindana na timu kama TP mazembe, Al Ahly, Mamelodi Sundown na vigogo wengine Afrika
Kwa mujibu wa Mo, michakato ya usajili inatarajiwa kuanza rasmi wiki inayoanza kesho na amesema kwanza wataanza na wachezaji waliomaliza mikataba
Usajili wa wachezaji wapya utazingatia mapendekezo a benchi la Ufundi, na amesisitiza watamsajili mchezaji yeyote aliyependekezwa na kocha Aussems
Kama mabosi wa Simba watatekeleza ahadi hii, basi msimu ujao Simba inaweza kuvuka malengo yake na kuwa mshindani kamili wa taji la ligi ya mabingwa
0 Comments