Windows

Stars yafanya maandalizi ya AFCON uwanja wa Taifa



Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kiliingia kambini juzi kujiandaa na michuano ya AFCON 2019 itakayofanyika Misri kuanzia Juni 21 2019

Stars iliyoweka kambi Hoteli ya Whitesands, inafanya mazoezi kwenye uwanja wa Taifa ambapo baadhi ya wachezaji walianza mazoezi jana
Baadhi ya nyota wa timu hiyo jana walishiriki kwenye mchezo wa hisani kati ya Marafiki wa Mbwana Samatta na Marafiki wa Ali Kiba mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa na Marafiki wa Samatta kuibuka na ushindi wa mabao 6-3

Wachezaji wote 39 walioteuliwa na kocha Emmanuel Amunike wanashiriki kwenye mazoezi hayo mpaka Juni 07 ambapo wachezaji saba watachujwa tayari kwa safari ya kuelekea nchini Misri


Juni 13 Stars itajipima katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Misri, wenyeji wa michuano hiyo
Mechi ya kwanza ya Stars itapigwa Juni 23 dhidi ya Senegal, moja ya timu zinazopewa nafasi ya kufanya vizuri kwenye michuano hiyo
Kikosi cha Senegal kitaongozwa na mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane ambaye aliibuka mfungaji bora wa ligi kuu ya Uingereza sambamba na Pierre Emerick Aubemeyang na Mohammed Salahcut
Mbali na Senegal, Stars iko kundi C na timu za Algeria na Kenya
Ili kuweza kufanya vizuri katika kundi hili, Stars inahitaji kufanya maandalizi kabambe kwani ukiondoa Kenya, Senegal na Algeria ni timu ambazo zimekamilika zikiwa na nyota wengi wanaosakata kabumbu barani Ulaya
Tanzania inachukuliwa kama 'under-dog' wa kundi hili

Post a Comment

0 Comments