Mkoa wa Simiyu umekuwa ni mkoa wa kwanza Tanzania kuanzia shule ya kwanza ya umma itakayokuwa na jukumu la kuendeleza michezo na elimu nchini.

Taarifa hiyo imetolewa wakati wa ufunguzi wa mashindano ya UMITASHUMTA yanayofanyika njini Mtwara ambapo Waziri Harrison Mwakyembe ameupongeza kwa hatua hiyo.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Jumanne Sagini amesema kuwa mkoa wa Simiyu uliamua kuja na wazo la kuanzisha shule ya michezo kwa lengo la kulea vipaji vya michezo shuleni.

Amesema kuwa shule hiyo inatarajiwa kuanza mwaka ujao wa masomo ambapo wataanza kwa kuchukua watoto 120 katika mwaka wa kwanza na baada ya hapo watakuwa wakichukua wanafunzi 80 kila mwaka.

“Shule hii zamani ilikuwa ni ya kutwa tumeigeuza kuwa ya bweni na inaitwa shule ya sekondari Simiyu, na tunatarajia kuwa na jumla ya wanafunzi 320 ambapo vijana watakaokuwa wakifaulu mitihani yao ya darasa la saba na wenye vipaji vya michezo wataletwa moja kwa moja katika shule hii,” amesema.